
Mungu wangu, nakupenda sana Wewe ni Alfa na Omega Umenishika hata nilipochoka Umeniinua tena kila mara Tunakusifu, Yesu mwema Mioyo yetu iko mikononi mwako Umetulinda, umetupitisha Kwenye machozi na kwenye mashaka Tunarudisha shukrani Kwa neema zako zilizojaa kila siku Tunarudisha shukrani Kwa rehema zako zisizokwisha Wewe ni Baba wa milele Mkombozi wetu, mwamba wetu Tutaimba jina lako daima Mungu wetu, tunakuabudu

